TETESI: Stopper, Onyango anga za Simba, Karihe na Mashujaa…
Simba imefanya mazungumzo ya kumpata beki wa KVZ ya Zanzibar, Salum Athuman ‘Stopper’ ambaye amekuwa na kiwango bora. Zao hilo la timu ya vijana ya Simba, aliyewahi kucheza pia Fountain Gate, JKT TZ na Mbeya Kwanza, amekuwa katika kiwango bora na ikielezwa Msimbazi walimfuatilia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi na Muungano iliyofanyika mwaka huu…