Simba Queens mabingwa WPL 2023/24, yakata tiketi ya Ligi ya Mabingwa
SIMBA Queens imekata tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) kwa wanawake baada ya leo kuifunga Alliance Girls mabao 3-0, kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza na kubeba ubingwa wa Ligi Kuu uliokuwa ukishikiliwa na JKT Queens msimu uliopita. Mabao ya straika Jentrix Shikangwa aliyeweka kambani mara mbili na akifikisha mabao 10 na…