Wataka wajumbe kuondolewa uchaguzi wa madiwani, wabunge CCM
Babati. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimechukua na kinakwenda kufanyia kazi mapendekezo ya wanachama wake mkoani Manyara wanaotaka wagombea udiwani na ubunge kuchaguliwa na wanachama na si wajumbe. Ushauri huo wameutoa leo Jumamosi, Juni 1, 2024 katika mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya zamani ya Babati Mjini, uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk…