Wafugaji watajwa tembo kuvamia makazi ya watu
Dodoma. Wakati vilio vya wanyama waharibifu wakiwemo viboko, tembo na nyani kuvamia makazi ya watu vikisikika bungeni, wafugaji wanatajwa kuchangia hali hiyo. Wabunge pia wamepigia kelele fidia kwa wananchi wanaopata madhara kutokana na wanyama hao, wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2024/25. Wamechangia mjadala…