Dk Biteko atoa maagizo Ewura, asifu utekelezaji wa kazi

Tanga. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), kuhakikisha upatikanaji endelevu wa mafuta kwa gharama halisi, kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya sheria, na kushughulikia malalamiko ya wateja kwa haraka ili kuboresha huduma kwa Watanzania. Dk Biteko ametoa maagizo…

Read More

MAKAMU WA RAIS AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU NKONDO

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na mwenza wake Mama Mbonimapaye Mpango wameifariji familia na waombolezaji mbalimbali kufuatia kifo cha Bw. Johnson Nkondo aliyekuwa Msaidizi wa Ofisi Mkuu – Ofisi ya Makamu wa Rais aliyefariki tarehe 13 Februari 2025 katika Hospitali ya Benjamini Mkapa mkoani Dodoma…

Read More

WANANCHI WAASWA KUKOPA KWENYE VIKUNDI VILIVYOSAJILIWA

    Na. Eva Ngowi, WF, KILIMANJARO Serikali imewaasa wananchi kuepuka kukopa fedha kwenye Taasisi ama vikundi vinavyotoa huduma za kifedha bila kusajiliwa rasmi kwa mujibu wa sheria ili kuepuka athari zinazoambatana na mikopo umiza. Tahadhari hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Vijijini Bw. Shadrack Mhagama, katika kikao kilichofanyika ofisini kwake…

Read More

Kipindupindu chaua wawili Mara, RC atoa maagizo kwa Ma-DC

Musoma. Watu wawili wamefariki dunia, huku wengine 140 wakiugua ugonjwa wa kipindupindu katika Wilaya za Musoma na Rorya, mkoani Mara. Ugonjwa huo umeibuka katika wilaya hizo tangu Januari 23, 2025, huku chanzo kikuu kikitajwa kuwa ni matumizi hafifu ya vyoo safi na salama katika maeneo yaliyoathiriwa na ugonjwa huo. Hayo yamesemwa leo, Jumatatu, Februari 17,…

Read More

Mabadiliko ya sheria yapendekeza NHC ipewe ruzuku

Dar es Salaam. Serikali imependekeza kufanya mabadiliko ya vifungu 20 vya Sheria ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Sura ya 295 ili kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wake. Miongoni mwa maeneo yaliyoguswa ni kuongeza ruzuku kama chanzo cha mapato cha NHC, mwajiri kuondolewa uwezo wa kukata kiasi cha pesa kama kodi ya nyumba…

Read More

Wanaotoa mikopo umiza ujumbe wenu huu hapa

Geita. Serikali imezitaka kamati za ulinzi na usalama kuwachukulia hatua kali wale wanaotoa mikopo bila kuwa na leseni, pamoja na kuwanyang’anya leseni hizo wote wanaotoa mikopo bila kuzingatia masharti na kuwaumiza wananchi. Mikopo hiyo, ambayo imepachikwa majina mengi ikiwemo kausha damu, komandoo, pasua moyo, kichefuchefu na mengine mengi, imekuwa ikitajwa kuwa chanzo cha kufilisika, kujiua,…

Read More

Chunya kuzalisha kilo milioni 31 za tumbaku 

Mbeya. Jumla ya kilo milioni 31 za tumbaku zinatarajia kuzalishwa mkoani hapa  kwa msimu wa kilimo 2025/26 sambamba na uanzishaji wa mfuko wa majanga kwa wakulima. Uzalishaji huo umetajwa kuongezeka kutoka wastani wa kilo milioni 19 zilizopatikana msimu wa kilimo 2024/25 kati ya kilo milioni 26 zilizotarajiwa kuzalishwa. Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Februari 17,…

Read More

Upelelezi kesi ya kumiliki mijusi 226 bado

Dar es Salaam. Upelelezi wa kesi mbili za kumiliki mijusi 226 aina ya Coud Gecko yenye thamani ya Sh13.8milioni, inayomkabili mfanyabiashara, Hika Shabani Hika (48) maarufu Majoka na Shaban Salum Mzomoke (45) maarufu kama Kisukari, haujakamilika. Wakili wa Serikali, Frank Rimoy ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Februari 17, 2025 wakati kesi hizo zilipoitwa…

Read More

Matumizi ya drone kuongeza uzalishaji wa pamba Maswa

Maswa. Matumizi ya teknolojia ya kisasa ya ndege zisizo na rubani (drone) katika kunyunyizia dawa kwenye zao la pamba yanatarajiwa kuongeza uzalishaji kutoka tani 13 katika msimu wa mwaka 2023/2024 hadi tani 50 katika msimu wa mwaka 2024/2025. Hayo yameelezwa leo, Februari 17, 2025, na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge, katika Kijiji cha…

Read More