Bodi ya mikopo yavuna faida Sh1.5 trilioni ndani ya miaka 20

Dar es Salaam. Zaidi ya Sh1.5 trilioni imetengenezwa kama faida na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kupitia mikopo ya Sh8.2 trilioni iliyotolewa kwa wanafunzi. Faida hiyo imepatikana kupitia mikopo iliyowanufaisha zaidi ya wanafunzi 830,000 waliosoma katika ngazi mbalimbali ndani ya miaka 20. Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati wa kilele…

Read More

Daraja linalounganisha Tabora, Shinyanga kuondoa kero

Kahama. Ujenzi wa daraja linalounganisha mikoa ya Shinyanga na Tabora katika Mto Kasenga linatajwa kuwa suluhisho la usafiri na kuondoa kero kwa wananchi wa mikoa hiyo. Hayo yameelezwa na Mhandisi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Shinyanga, Evans Maridai leo Februari 17, 2025 akisema kwa sasa upasuaji wa miamba umekamilika. “Daraja hili lina…

Read More

Tanzania itakavyopunguza foleni katika miji na majiji

Dodoma. Serikali imetangaza mpango mahususi wa kukabiliana na msongamano wa magari katika majiji matano na miji mitatu nchini ikiwamo upanuzi wa barabara zinazoingia katika maeneo hayo. Misururu ya magari imekuwa kawaida kuonekana asubuhi na jioni wakati watu wakielekea na kutoka kazini. Foleni zimekuwa ni za kawaida katikati ya majiji au miji inayokua. Kiafya, foleni pia…

Read More

Kicheko kwa wanaume wenye vipara

Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Sheffield, Uingereza na wenzao kutoka Chuo Kikuu cha COMSATS nchini Pakistan, ndio waliogundua mafuta hayo. Kwa mujibu wa utafiti huo, mafuta yenye sukari (deoxyribose sugar) yana kemikali ya kaboni ambayo inasaidia kutokomeza upara. Wanasayansi waligundua hilo kibahati baada ya kuyapaka mafuta hayo kwenye sehemu ya mwili wa panya aliyekuwa amejeruhiwa…

Read More

Mapya Wapakistan wanaodaiwa kusafirisha dawa za kulevya

Dar es Salaam. Wakati Serikali ikiendelea na uchunguzi wa kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine na Methamphetamine zenye uzito wa kilo 447.3 inayowakabili raia nane wa Pakistan, washtakiwa hao wamedai kuwa hawana nguo za kubadilisha huko gerezani. Pia, washtakiwa hao wamedai hawana mawasiliano na familia zao zilizopo Pakistan, tangu walipofikishwa mahakamani hapo….

Read More

Sababu barafu kupungua Mlima Kilimanjaro – 1

Kilimanjaro. Desemba, 2024, nilipanda Mlima Kilimanjaro, ambao barafu yake inapungua kadri miaka inavyosonga. Sababu kubwa ikitajwa ni mabadiliko ya tabianchi, na baadhi ya watu wanahusisha na matukio ya moto mlimani. Safari ilianza Marangu ambako nilikatiza msitu wenye miti mingi ya asili (msitu mnene). Kulingana na msimu, kulikuwa na mvua. Kutoka Mandara, niliingia eneo la uwanda…

Read More

Hivi ndivyo Kariakoo ya saa 24 itakavyokuwa

Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki siku 10 eneo la kibiashara Karikaoo jijini hapa kuanza kufanya kazi saa 24, wafanyabiashara wameeleza namna walivyojiandaa ukiwamo ushiriki katika ulinzi, usalama wao na wa wateja. Januari 30, 2025 akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa Dar es Salam, Albert Chalamila alisema uzinduzi rasmi wa kufanyika biashara…

Read More