Watatu kortini wakidaiwa kusafirisha kilo 145 za mirungi
Dar es Salaam. Said Ndomboloa na wenzake wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina mirungi zenye uzito wa kilo 145.20. Mbali na Ndombokoa, washtakiwa wengine ni Hamisi Ndomboloa na Amor Seiph. Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatatu, Februari 17, 2025, na kusomewa mashtaka…