Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema taifa linapitia kipindi kigumu kutokana na vifo na uharibifu wa mali vilivyoripotiwa katika vurugu za siku ya uchaguzi Oktoba 29, 2025, na kwamba hatua za msingi zimeanza kuchukuliwa ili kurejesha maelewano na amani.
Akizungumza Ijumaa, Novemba 14, 2025, wakati akilifungua Bunge la 13 jijini Dodoma, Rais Samia ameanza hotuba yake kwa kuwataka wabunge na wageni kusimama kwa dakika moja kuwaombea watu waliopoteza maisha.
Rais Samia ameongeza kuwa amehuzunishwa binafsi na matukio hayo, akitoa pole kwa familia zilizoondokewa na wapendwa wao, majeruhi na wale walioathiriwa kwa uharibifu wa mali.
Ameeleza kuwa Serikali tayari imeunda Tume inayochunguza chanzo na mtiririko wa matukio hayo, ili kutoa mwongozo wa hatua zitakazosaidia kurejesha utulivu.
Related
