
Benchikha na msala wa 5-1 za Yanga SC
Ilikuwa Novemba 5, 2023 uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Yanga iliichapa Simba mabao 5-1 kwenye mechi ya ligi na kupelekea kufutwa kazi kwa aliyekuwa kocha mkuu wa wekundu wa Msimbazi, Roberto Oliveira ‘Robertinho’. Ni mechi iliyokuwa na hisia mbili tofauti. Furaha kwa wageni Yanga. Huzuni kwa kwa wenyeji Simba. Iliichukua Yanga dakika tatu kuandika bao…