
Sh900 milioni zaboresha Hospitali ya Wilaya Nachingwea
Nachingwea. Serikali imetoa Sh900 milioni kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya katika hospitali kongwe ya Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi. Fedha hizo zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya kisasa, kichomea taka ambacho kinatumia umeme na mafuta, jengo la kufulia nguo na la wagonjwa wa nje…