
Polisi yawashikilia watu 21 wakituhumiwa kwa uhalifu
Unguja. Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi linawashikilia watuhumiwa 21 wakidaiwa kujihusisha na matukio ya wizi, uporaji na unyang’anyi wa kutumia mapanga. Watuhumiwa wamekamatwa baada ya polisi kufanya oparesheni maalumu ya kuwasaka watu wanaojihusisha na matukio ya uhalifu. Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 16, 2024 ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi,…