Admin

Chalamila atishia kumweka ndani mkandarasi mwendokasi

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema haridhishwi na kasi ya ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka ya Gongo la Mboto. Amesema kama hali itaendelea hivyo, atamweka ndani mkandarasi au mhandisi mshauri. Ametoa kauli hiyo leo Aprili 18, 2024 alipofanya ziara kukagua ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu…

Read More

Sababu Rais Samia kupewa shahada nne za heshima

Dar es Salaam. Uimara katika usimamizi wa sekta fulani na kuwa na mchango katika Taifa lake ni miongoni mwa sababu zilizotajwa na wasomi kuwa chachu ya Rais Samia Suluhu Hassan kutunukiwa shahada ya nne ya heshima ya udaktari. Kwa mujibu wa wasomi hao, mara nyingi shahada hizo hutolewa kwa mtu aliyeonyesha mchango mkubwa katika Taifa…

Read More

Dk Nchimbi atoa agizo Wizara ya Kilimo

Mbeya. Wakati Serikali ya Tanzania ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya ardhi ya kilimo wilayani Mbarali, Wizara ya Kilimo imeagizwa kufanya mazungumzo na mmoja wa wamiliki wa mashamba makubwa ili kuachia moja ya maeneo yake kwa ajili wakulima wa Mlonga na Mnazi. Agizo hilo limetolewa leo Alhamisi, Aprili 18, 2024 na Katibu Mkuu wa Chama…

Read More

Makete mpya isiyo na vilio vya misiba tena

Njombe, Makete. Takriban miongo miwili iliyopita ilikuwa ni jambo la kawaida kuzika watu watatu mpaka wanne kwa siku waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) wilayani Makete. Wilaya hiyo ni miongoni mwa zilizoathiriwa zaidi na maambukizi VVU nchini na kupitia wakati usioelezeka, hasa ilipofikia hatua ya viongozi wa kaya (baba na mama) kufariki…

Read More

Hatari ya shisha kwa vijana katika kifua kikuu

Dar/Mikoani. Ni kawaida siku hizi katika kumbi za starehe mijini kukuta mitungi ya shisha juu ya meza, huku watumiaji wakichangia kilevi hicho. Je, unajua kuna uwezekano mkubwa mtumiaji kupata maambukizi ya Kifua Kikuu (TB)? Ijapokuwa hakuna utafiti wa moja kwa moja Tanzania unaoonyesha shisha ni chanzo cha TB, nchini Uswizi kupitia utafiti uliofanywa na Dk…

Read More

Hali tete wajawazito Temeke, uongozi wataja mikakati

Dar es Salaam. Idadi kubwa ya wajawazito wanaopokewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke imesababisha wachangie kitanda kimoja wawili hadi watatu. Licha ya changamoto hiyo, wajawazito hao, wengi wakiwa ni wenye rufaa wanasema kikubwa kwao ni kupata matibabu ya kibingwa. Hata hivyo, Serikali inafanya jitihada mbalimbali kukabiliana na hali hiyo ikiwa ni pamoja…

Read More

Baba Sure Boy auweka mpira kati Kariakoo Dabi

Abubakar Salum ‘Sure Boy Sr’ ambaye ni baba mzazi wa kiungo wa Yanga, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amesema Kariakoo Dabi haijawahi kutabirika, haijalishi ni timu gani inakuwa kwenye kiwango kizuri kwa wakati huo. Mkongwe huyo aliyewahi kuichezea Yanga SC, amesema kwenye makaratasi Yanga imeonyesha kiwango cha juu kwenye mechi mbalimbali, lakini hilo halitoshi kuona ni…

Read More

Serikali kupanua mkongo wa Taifa kuboresha mawasiliano

Mwanza. Wakati baadhi ya wananchi wakilalamikia gharama za vifurushi vya intaneti kuwa juu, Shirika la Mawasiliano nchini (TTCL) limeanza kupanua mkongo wa Taifa na kuuongezea uwezo wake ili kufikisha mawasiliano pande zote nchini kwa gharama nafuu. Wakizungumza leo wakazi wa mkoani Mwanza wamesema bei za vifurushi vya intaneti zinawaumiza hasa wajasiriamali wanaofanya shughuli zao mitandaoni….

Read More

Rais Mwinyi: Serikali zinaendelea kushughulikia changamoto za Muungano

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema Serikali zote za Tanzania na Zanzibar mbili zinaendelea kuchukua hatua mbalimbali kushughulikia na kupata ufumbuzi wa changamoto za Muungano zinazojitokeza. Amesema utatuzi wa changamoto hizo umezidi kujenga imani kubwa kwa wananchi kuhusu uimara wa Muungano huo. Kwa nyakati mbalimbali juhudi zimekuwa zikichukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya…

Read More