
Serikali kupanua mkongo wa Taifa kuboresha mawasiliano
Mwanza. Wakati baadhi ya wananchi wakilalamikia gharama za vifurushi vya intaneti kuwa juu, Shirika la Mawasiliano nchini (TTCL) limeanza kupanua mkongo wa Taifa na kuuongezea uwezo wake ili kufikisha mawasiliano pande zote nchini kwa gharama nafuu. Wakizungumza leo wakazi wa mkoani Mwanza wamesema bei za vifurushi vya intaneti zinawaumiza hasa wajasiriamali wanaofanya shughuli zao mitandaoni….