
Namna makachero walivyomdaka mwizi wa bastola
Moshi. Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Benedicto Petro aliyeongoza timu ya makachero kuwakamata washtakiwa wa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, ameeleza namna walivyomkamata mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Eben Mwaipopo. Mshitakiwa huyo alikamatwa katika Kituo cha Basi cha Bomang’ombe wilayani Hai. Shahidi ameeleza kuwa, katika mahojiano, mshitakiwa aliwaeleza alipoificha silaha iliyotumika katika mauaji mkoani…