
Wawili wafariki dunia kwa kufukiwa na kifusi kwenye mgodi usio rasmi
Geita. Wachimbaji wawili (maarufu Manyani) wamepoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba dhahabu kwenye machimbo yasiyo rasmi yaliyopo Magenge wilayani Geita mkoani hapa. Mkaguzi Msaidizi kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, Wambura Fidel amesema vifo hivyo vimetokea Juni 5,2024 baada ya wachimbaji hao kuingia kwenye eneo lenye leseni ya utafiti na…