
Singida Black Stars, KMC vita mpya Ligi Kuu Bara
UTAMU wa Ligi Kuu Bara unaendelea tena leo kwa michezo miwili, huku macho ya mashabiki yakiwa kwenye Uwanja wa Liti mjini Singida wakati Singida Black Stars itakapovaana na KMC, huku kocha Patrick Aussems akitamba kuendeleza ubabe. KMC mazoezini Singida ilianza msimu kwa kishindo kwa kupata ushindi katika mechi mbili mfululizo ikiwa ugenini, ikianza kwa kuichapa…