Wandewa wanaingia, Yanga | Mwanaspoti

“EEEH! Wandewa wanaingia … Ooh wenye mji wamevamia.” Hiyo ni mistari iliyopo katika ngoma moja matata ya Achii aliyoimba Diamond Platinumz akimshirikisha Koffi Olomide. Baada ya kushuhudiwa mechi 10 za Ligi Kuu Bara, leo zinapigwa mechi mbili ikiwamo ile itakayokutanisha watetezi, Yanga dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba ma mapema KMC itakuwa wenyeji wa Coastal…

Read More

Simba yarudi njia kuu, Ahoua mdogomdogo

SIMBA ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kushinda mechi mbili za awali kwa kishindo na kuvuna pointi sita na mabao saba, na kufanya mashabiki wa timu hiyo kutamba “Chama ndo limerudi njia kuu?” Simba ilianza kwa kuishindilia Tabora United kwa mabao 3-0 kisha kuizima Fountain Gate kwa mabao 4-0 na kukaa…

Read More

Maestro: Azam FC tatizo kila msimu ina timu mpya

Mchezaji wa zamani na mchambuzi wa soka, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ amesema kutolewa kwa timu za Zanzibar za JKU na Uhamiaji kunatokana na ubora mdogo wa wachezaji, wakati Azam wao wakisumbuliwa na kukosa muunganiko. Maestro, aliyewahi kuichezea KMKM ya Zanzibar amesema timu za visiwani humo zina tatizo la ubora mdogo wa wachezaji tofauti na zamani ambako…

Read More

Mwita: Azam iongeze mashabiki ipate presha ya matokeo

MKURUGENZI wa Fedha na Mipango wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF), Awadh Maulid Mwita amewataka Azam FC kuongeza wigo wa mashabiki wa timu yao ili ipate presha ya kusaka matokeo chanya kwenye mechi zao. Mwita ameyabainisha hayo leo Agosti 28, 2024 wakati akichangia kwenye mjadala wa Mwananchi Space, inayoandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL) wenye…

Read More

Kufeli klabu nne CAF tatizo uwekezaji

MDAU wa michezo Masanja Ngwau, ameeleza tatizo kubwa lililozikumba timu nne zilizotolewa mapema kwenye mashindano ya Afrika kwa klabu ni uwezekezaji duni. Masanja amesema klabu za Zanzibar na hata ile moja nje ya Azam, zimekumbana na kutolewa raundi ya awali kutokana na kukosa maandalizi mazuri ya mashindano hayo na kujikuta zinatolewa mapema. Mdau huyo ameyabainisha…

Read More

Gambo Jr: Azam FC ikaombe msamaha ilikokosea

MDAU wa soka nchini, Hosea Gambo Paul ‘Gambo Jr’ amesema kama kuna sehemu Azam FC ilikosea ni vyema ikaenda kuomba msamaha kutokana na kushindwa kufanya vyema katika michuano ya kimataifa, kwani ni klabu iliyokamilika kwa kila kitu. Gambo ameyabainisha hayo leo Agosti 28, 2024 wakati anachangia mada kwenye mjadala unaoendeshwa na Mwananchi X Space unaohoji…

Read More

Mdau: Bado hatujawa tayari  katika ushiriki wa kimataifa

RAMADHAN Elias ambaye ni mdau wa michezo, amesema ishu kubwa ambayo inazitesa timu za Tanzania katika michuano ya kimataifa ni kutokuwa tayari. Elias ameyabainisha hayo leo Agosti 28, 2024 wakati akichangia mada katika Mwananchi Space, inayoandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL) isemayo: “Tumekosea wapi timu nne za Tanzania kutolewa mashindano ya klabu Afrika?” Mdau huyo…

Read More

Kakolanya asimulia kipigo cha kwanza

KIPA wa Namungo FC, Beno Kakolanya amesema kuanza kwao vibaya mechi ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya Tabora United iliyowafunga mabao 2-0, imewafungua macho kukaza buti. Alisema Tabora United ilikuwa na kikosi cha wachezaji wazuri kama mshambuliaji Heritier Makambo, hivyo ushindani ulikuwa mkubwa ambao uliwapa wapinzani wao ushindi. “Hakuna kitu kibaya kama kufungwa nyumbani,…

Read More

Makambo aongeza mzuka Tabora United

UWEPO wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Heritier Makambo ndani ya kikosi cha Tabora United, umeonekana kuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo. Mashabiki hao wamesema Makambo ameongeza staili ya tatu ya kushangilia kutoka mbili walizozizoea. Tambo hizo zinakuja ikiwa ni siku chache baada ya timu yao kuichakaza Namungo mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara…

Read More

Yusuph: CAF yapo mengi ya kujifunza

MSHAMBULIAJI wa Coastal Union, Mbaraka Yusuph amesema licha ya kutolewa katika hatua za awali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF), lakini hawajatoka patupu. Coastal ilitolewa katika mashindano hayo baada ya kufungwa nyumbani na ugenini jumla ya mabao 3-0 na Bravos do Maquis ya Angola, jambo ambalo mchezaji huyo kalichukua kama funzo la kujituma…

Read More