
Mgomo wafanyika Israel kushinikiza kuachiliwa kwa mateka – DW – 02.09.2024
Wafanyakazi hao wanapinga hatua za serikali kushindwa kuumaliza mzozo huo na kufanikisha kuwarejesha nyumbani mateka waliosalia mikononi mwa kundi la Hamas. Mgomo huo unaoongozwa na muungano wa mashirika ya wafanyakazi ya Israel, Histadrut umekwamisha shughuli za kibiashara na kijamii. Idadi kubwa ya miji na jamii kadhaa zilijiunga na maandamano hayo, huku baadhi wakikataa kufanya hivyo…