
Urusi yaishutumu Marekani kuhusika na shambulizi la Crimea – DW – 24.06.2024
Akinukuliwa na Shirika la TASS, Msemaji wa serikali ya Urusi, Dmitry Peskov amesema wanajua dhahiri nani hasa ambae amehusika na shambulioa hilo, nani aliyelengwa na makombora hayo ya teknolojia ya kisasa na kwamba si Ukraine ambayo imehusika katika shambulio hilo. Bila kupindisha kauli msemaji huyo aliinyoshea kidole Marekani kwa kile alichokisema kuhusika moja kwa moja…