
Ma-DC watwishwa mzigo utatuzi wa migogoro familia, ardhi
Ruangwa. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamia utatuzi wa migogoro ya wosia, ardhi na ile ya kifamilia kwenye maeneo yao. Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia leo Februari 19 2025 katika uwanja wa Madini wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi….