
Serikali yaanza kumwaga fedha miradi ya barabara
Lindi. Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema Serikali imeanza kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi ya ujenzi wa barabara, hivyo hakutakuwa na kisingizio kwa makandarasi kutoikamilisha kwa wakati miradi hiyo. Waziri Ulega ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Januari 11, 2025 wakati akikagua ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Nachingwea – Ruangwa –…