
Ajali ya ndege yaua 241 India, mmoja anusurika
Ahmedabad. Mwaka 2025 umeendelea kuwa wa majanga kwa sekta ya usafirishaji wa anga duniani baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Air India yenye abiria na wahudumu 242 kuanguka eneo la makazi la Meghani Nagar nchini India. Ndege hiyo aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyokuwa safarini kutoka Ahmedabad India kuelekea jijini London nchini Uingereza…