NCCR yasema uchumi wake hauruhusu kufanya mikutano

Dar es Salaam. Viongozi wa Chama cha NCCR Mageuzi wametakiwa kurudi majimboni mwao ili kuwahamasisha wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa na kukijenga chama. Hatua ya chama hicho imekuja baada ya kile kinachoelezwa hali ya uchumi wa chama hicho kutowaruhusu kufanya  mikutano ya hadhara kama vyama vingine. Kuwaambia viongozi wao warudi majimboni ni moja…

Read More

Waziri Mkuu kuongoza majaribio SGR Dar-Dodoma Aprili 21

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza safari ya majaribio ya treni ya reli ya kisasa (SGR) itakayofanya safari kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ikiwa na watu takriban 600. Majaribio hayo yatafanyika Aprili 21, 2024.  Katika treni hiyo Majaliwa ataambatana na viongozi wa Serikali, dini na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenda Dodoma…

Read More

Aliyetishia Kariakoo Dabi mtandaoni adakwa na Polisi

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Abdulshahib Hegga ‘GB64’ kwa tuhuma za kuhamasisha watu kufanya vurugu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Simba kesho. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema shabiki huyo maarufu wa Simba…

Read More

Mbivu, mbichi suala la kikokotoo kujulikana Mei Mosi

Dodoma. Serikali imesema suala la kanuni mpya ya kikokotoo cha pensheni ya wastaafu lina maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan na limeanza kufanyiwa kazi, majibu yatajulikana kwenye sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, jijini Arusha. Hayo yamesema leo Ijumaa Aprili 19, 2024 na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira…

Read More

Wakongwe: Ni Dabi ya suluhu au sare

 Mastaa waliowahi kuzichezea Simba na go Yanga wametoa utabiri wa mechi ya Kariakoo Dabi ya Ligi Kuu Bara inayopigwa kesho, Jumamosi, uwanjani Benjamin Mkapa, wengi wao wakiiona suluhu au sare. Mzunguko wa kwanza Simba ikiwa mwenyeji wa mchezo ilifungwa mabao 5-1, lakini pamoja na hilo mastaa hao hawaoni kama linaweza likajirudia. Mwanaspoti limefanya mahojiano na…

Read More

Wafugaji Monduli walia bwawa kupasuka, kupoteza maji

Arusha. Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Nanja kilichopo wilaya ya Monduli mkoani Arusha, wameiomba Serikali kuharakisha ukarabati wa kuta za bwawa la maji lililopo kijijini hapo, ambalo kuta zake zimevunjika na kusababisha maji mengi kupotea. Bwawa hilo la kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kunyweshea mifugo, liliharibiwa na maji…

Read More

Aprili inavyoibeba Simba Kariakoo Dabi

MASHABIKI wa Simba na Yanga tayari viroho vimeanza kuwadunda, wakati wakiendelea kuhesabu siku kabla ya timu zao kushuka katika pambano la Ligi Kuu Bara litakalopigwa Jumamosi hii ya Aprili 20, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Hili litakuwa pambano la 112 kwa timu hizo kukutana katika Ligi Kuu Bara tangu mwaka 1965,…

Read More

Mtoto adaiwa kujinyonga Arusha kisa kuchelewa shule

Arusha. Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Olomitu iliyoko Chekereni jijini Arusha, Yusuph Zephania (13) anadaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kuogopa adhabu itakayotolewa kwake baada ya kuchelewa shule. Tukio hilo limetokea jana April 18, 2024 nje ya nyumba katika kamba ya kuanikia nguo iliyokuwa nje. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP…

Read More

Mambo 3 yanaibeba Yanga SC

JUMAMOSI ya wiki hii, inapigwa Kariakoo Dabi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga itakuwa mwenyeji wa Simba ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara. Kuanzia saa 11:00 jioni, ndiyo mchezo huo unatarajiwa kufanyika na kila upande unazihitaji alama tatu ili kujiwekea mazingira mazuri kunako ligi hiyo inayoelekea ukingoni. Yanga na Simba kila mmoja ameutolea macho…

Read More