
Kukazia hukumu kwatajwa kikwazo utoaji haki
Dar es Salaam. Wabunge wametaka utaratibu wa kukazia hukumu mtu anaposhinda kesi uangaliwe upya kwa kupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria bungeni. Wabunge Mashimba Ndaki wa Maswa Magharibi na Edward Ole Lekaita wa Kiteto wameitaka Serikali ibadilishe sheria ya kukazia hukumu wakisema ni mlolongo mrefu, badala yake mtu anaposhinda kesi akabidhiwe haki yake bila kuchelewa….