Wabunge wapaza sauti kukosekana haki mahakamani
Dodoma. Wabunge wametaka utaratibu wa kukazia hukumu pale mtu anaposhinda kesi ya madai uangaliwe upya kwa kupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria bungeni. Wabunge Mashimba Ndaki wa Maswa Magharibi na Edward Ole Lekaita wa Kiteto wametaka Serikali ibadilishe sheria ya kukazia hukumu, wakisema ina mlolongo mrefu, badala yake wanataka mtu anaposhinda kesi akabidhiwe haki yake…