Kamati kuu ya Chadema kukutana Mei 4

Dar es Salaam. Vigogo wa Chadema wanatarajia kujifungia katika kikao cha kamati kuu kinachotarajiwa kufanyika Mei 4 kikiwa na ajenda mbalimbali ikiwamo ya uchaguzi wa ndani wa chama hicho. Ajenda nyingine zitakazojadiliwa na vigogo hao ni tathimini ya wiki wa maandamano ya amani yaliyoingia siku ya saba leo, yenye lengo la kufikisha kilio cha wananchi…

Read More

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFANYA ZIARA KATIKA HOSPITAL YA WILAYA NA MNAZI MMOJA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akipokea maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa Hospital ya Wilaya wa Magharini “B” Mwanakwerekwe Ijitimai wakati alipofanya ziara ya  kutetembelea na kukagua utowaji wa huduma katika hospitali hio. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na wagonjwa waliolazwa katika wodi ya mifupa…

Read More

Pamba yasimamisha Jiji, yapokelewa kishujaa Mwanza

Mwanza. USIPIME! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na mapokezi makubwa iliyoyapata Pamba Jiji leo baada ya kupanda daraja kwenda Ligi Kuu Bara mwishoni mwa wiki iliyopita ikivunja mwiko wa miaka 23 tangu iliposhuka daraja mwaka 2001. Msafara wa timu hiyo uliokuwa umebeba wachezaji, benchi la ufundi na baadhi ya viongozi uliokuwa unatokea Arusha kupitia mkoani Shinyanga…

Read More

Warioba ataja sababu ya wapigakura wachache

Dodoma. Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba ametaja mambo ambayo yakifanyiwa kazi mapema yatawezesha wananchi wengi kushiriki uchaguzi na kuwapata viongozi wanaowataka kuwawakilisha kwenye vyombo vya maamuzi. Jaji Warioba ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 30, 2024 kwenye kongamano la wadau wa habari na uchaguzi Tanzania lililoandaliwa na baraza la habari nchini (MCT) Jijini Dodoma….

Read More

META KUTIA SAINI MAKUBALIANO YA UKODISHAJI NA UUZAJI WA VIFAA VYA UCHIMBAJI KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

Na Janeth Raphael -MichuziTv -Dodoma Mwakilishi kutoka Kampuni ya META Issa Mndeme amesema wapo katika hatua ya utiaji saini ya makubaliano ya ukodishaji na uuzaji vifaa vya uchimbaji kwa wachimbaji wadogo ili kuwasaidia kuepukana na changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakikumbana nazo kwenye uchimbaji. Mndeme ameyamesema hayo Jijini Dodoma kwenye mkutano wa kamati tendaji na Halmashauri…

Read More

Mtanda azikataa Simba, Yanga ndani ya Pamba

Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na mlezi wa timu ya Pamba Jiji, Said Mtanda amesema hatamvumilia mtu yeyote atakayeingiza U-Simba na U-Yanga ndani ya timu hiyo itakapokuwa inacheza mechi zake za Ligi Kuu Bara msimu ujao. Mtanda ametoa kauli hiyo leo Aprili 30, 2024 kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini hapa wakati akizungumza na maelfu…

Read More

LSF, Stanbic Tanzania kutekeleza miradi ya maendeleo

Dar es Salaam. Taasisi isiyo ya kiserikali ya The Legal Services Facility (LSF), kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic Tanzania, zimesaini makubaliano ya ushirikiano wa kutekeleza miradi ya maendeleo yenye lengo la kuwainua wanawake na wasichana kiuchumi, kielimu na kiafya. Mkataba huo wa miaka miwili unalenga kuweka juhudi na rasilimali za pamoja kati ya taasisi…

Read More