Miili miwili ya walioangukiwa na ukuta yazikwa Dar
Dar es Salaam. Miili ya watu wawili kati ya wanne wa familia moja waliofariki dunia kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba waliyokuwa wakiishi imezikwa. Ajali hiyo ilitokea Mtaa wa Goroka B, Toangoma, mkoani Dar es Salaam. Miili mingine imesafirishwa kwenda mkoani Kigoma. Ajali ilitokea asubuhi ya Aprili 26, 2024. Waliofariki dunia ni Lidya Heza (21),…