LENGO LA SERIKALI NI KUBORESHA MAISHA YA KILA MWANANCHI TARAFA YA NGORONGORO-NCAA
Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesema kuwa ina lengo la kuboresha maisha ya wananchi wa tarafa hiyo kwa kuwaelimisha na kuwahamisha wananchi waliojiandikisha kuhama kwa hiyari kwenda Kijiji cha Msomera Handeni Mkoani Tanga na maeneo mengine nchini. Akizungumza na wananchi wa tarafa ya Ngorongoro kwa nyakati tofauti katika zoezi la uelimishaji, uhamaishaji…