Wizara ya Madini kuwezesha wachimbaji wanawake, vijana

Dodoma. Wakati Wizara ya Madini imekuja na programu ya ‘madini ni mwanga kesho’ (MBT) kwa vijana na wanawake, pia imeliomba Bunge kuridhia bajeti ya Sh231.9 bilioni. Hayo yamesemwa leo Jumanne, Aprili 30, 2024 na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Mavunde amelieleza Bunge…

Read More

Bashungwa aagiza kukamatwa kwa mkandarasi anayejenga daraja la Mpiji chini – Dar

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amemuagiza Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni (OCD), Mohamed Senkondo, kumshikilia Meneja Mradi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group (CRSG), anayetekeleza ujenzi Daraja la Mpiji Chini (mita 140) pamoja na barabara unganishi (km 2.3), ahojiwe ili kuanza kuchukuliwa hatua kwa kuchelewa kuanza ujenzi wa daraja hilo na barabara unganishi….

Read More

Bunifu 42 za Kitanzania tayari kwenda sokoni

Dodoma. Bunifu na teknolojia 42 kati 283, zilizoibuliwa kupitia Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) na kuendelezwa kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech),  zimefikia hatua ya kuingia sokoni. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga amesema hayo leo Jumanne Aprili 30, 2024 alipokuwa akijibu swali la msingi…

Read More

LSF YATIA SAINI PAMOJA NA BENKI YA STANBIC TANZANIA KULETA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI WA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Jumatatu, Aprili 29, 2024 – Dar es Salaam, Taasisi isiyo ya kiserikali ya The Legal Services Facility (LSF), kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic Tanzania, zimesaini makubaliano ya ushirikiano wa kutekeleza miradi ya maendeleo yenye lengo la kuwainua wanawake na wasichana kiuchumi, kielimu na kiafya. Mkataba huu wa miaka miwili unalenga katika kuweka juhudi na…

Read More

PUMZI YA MOTO: Mkasa wa Pamba FC kushuka daraja 2001

HATIMAYE Pamba ya Mwanza imefanikiwa kurudi Ligi Kuu Bara tangu ishuke daraja 2001. Klabu hiyo ambayo sasa inatambulika kama Pamba Jiji, imepanda baada ya ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Mbuni ya Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini humo. Pamba, klabu yenye rekodi yake barani Afrika inarudi Ligi Kuu baada ya kukaa chini…

Read More

Watendaji watakiwa kusimia mfumo wa Force Account

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Ngubiagai amewatala Maafisa Tarafa na Watendajo wa Kata kuhakikisha wanasimamia kikamilifu matumizi ya mfumo wa Force Account ili kuondoa hoja za ukaguzi katika ngazi ya msingi. Mhe. Ngubiagai ametoa kauli hiyo tarehe 29 Aprili, 2024 wakati akifunga mafunzo kwa Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata Mkoa wa Mwanza…

Read More

Wanasheria Tanzania wapewa ujuzi kukabili uhalifu mtandao

Dar es Salaam. Ili kuimarisha utaalamu na mbinu za kisheria katika kukabiliana na uhalifu wa mtandao, Serikali inashirikiana na Urusi kubadilishana uzoefu na elimu juu ya masuala hayo. Katika kufanikisha hilo, wataalamu kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Urusi wamewasili nchini na kutoa mafunzo kwa wanafunzi na wanataaluma ya sheria kuhusu masuala hayo. Ushirikiano…

Read More