
Serikali kuunda timu tatu kuelekea Afcon 2027
Dodoma. Serikali ina mpango wa kuunda timu tatu imara za soka za Taifa kulingana na umri ambazo zitashiriki mashindano ya Afcon 2027 na mengine ambayo nchi itashiriki. Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amesema hayo leo Jumatatu Aprili 30, 2024 alipojibu maswali ya nyongeza ya Mbunge wa Jimbo la Magomeni, Mwanakhamis Kassim…