Makada Chadema kumkabili Lema Kaskazini
Mbeya. Wakati vigogo wa Chadema Kanda za Victoria, Serengeti, Nyasa na Magharibi wakipigana vikumbo kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi, baadhi ya makada wa Kanda ya Kaskazini nao wanajipanga kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Chadema, uchaguzi wa kanda nne utafanyika Mei mwaka huu na nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo…