
Tanesco kuajiri 430, wamo mafundi mchundo
Dodoma. Bunge limeelezwa kuwa watumishi 430 wataajiriwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) katika mwaka 2024/25. Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema hayo leo Ijumaa Aprili 19, 2024 alipojibu swali la mbunge wa Tunduru Kusini, Daimu Mpakate. Mbunge huyo amehoji ni lini Serikali itaajiri madereva na mafundi ambao wamekuwa vibarua wa muda mrefu kwenye…