Huduma ya maji yarejeshwa Hanang, wakazi 26,900 kunufaika
Hanang. Baada ya uharibifu wa miundombinu ya maji Wilaya ya Hanang mkoani Manyara uliosababishwa na maporomoko ya udongo, Shirika la WaterAid Tanzania limekarabati chanzo cha maji cha Nangwa kinachotegemewa na wananchi 26,900. Desemba 3, 2023, yalitokea mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyoambatana na mawe, magogo na maji kutoka Mlima Hanang na kusababisha vifo vya watu…