
Makabiliano kati ya jeshi na RSF yazuka upya Sudan – DW – 13.05.2024
Kulingana na Umoja wa Mataifa, watu 27 wamefariki dunia baada ya machafuko ya siku moja tu. Walioshuhudia wameripoti mashambulizi ya angani, makombora na makabiliano ya risasi yakirindima katika mji wa El-Fasher tangu Ijumaa iliyopita, ambapo taarifa ya Umoja wa Mataifa inasema makabiliano yaliyodumu kwa saa nzima yalisababisha watu 850 kuachwa bila makao. Umoja wa Mataifa…