
BALOZI MBAROUK AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ETHIOPIA JIJINI DODOMA
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Balozi Birtukan Ayano ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma. Katika mazungumzo yao viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Ethiopia kwa manufaa ya pande zote mbili….