alishawahi kufikiria kwamba itafika siku ambayo vile unavyolinda simu
yako dhidi ya uhalifu wa mtandaoni ndivyo itakavyokuja kuwa sawa na kwa
luninga yako?
Ndiyo,
 luninga yako nayo inahitaji ulinzi wa taarifa zako za siri, kama
ulikuwa haufahamu au hautilii maanani basi leo utajifunza kitu.
Maendeleo
 ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yamepelekea mwingiliano
 wa vifaa tofauti vya kidigitali vinavyounganishwa na mtandao wa
intaneti. Kwa mfano, sasa mtu anaweza kusimamia na kufuatilia mwenendo
wa matumizi ya vifaa tofauti vya umeme nyumbani kwake kama vile luninga,
 mashine ya kufulia, na kiyoyozi mahali na muda wowote alipo.
Mwingiliano
 huu humlazimu mtumiaji wa vifaa kuweka taarifa zake za siri ili kuweza
kuunganishwa navyo na hatimaye kuvisimamia kwa urahisi mahali popote
alipo. Hivyo mtu hujikuta anaingiza taarifa zake binafsi kama vile
majina, namba za simu, barua pepe, pamoja na nywila.
Bila
 shaka hii ni faida nyingine inayotokana na maendeleo ya teknolojia na
mawasiliano. Lakini tunajilindaje dhidi ya hatari zinazokuja na
mabadiliko haya? Watu wengi hudhani kwasababu luninga ni kifaa ambacho
tunakitumia na kukiacha nyumbani au sehemu zetu kazi basi hakipo
hatarini kushambuliwa na uhalifu wa mtandaoni.
Ukweli
 ni kwamba tunapaswa kuwa makini na uhakika wa usalama wa taarifa zetu
binafsi katika vifaa vyote vya kiteknolojia na mawasiliano
tunavyovitumia.
Kampuni ya Samsung kwa kuliona hilo mwaka 2013 ilitambulisha programu ya Knox kwa ajili ya kulinda mifumo ya uendeshaji na vifaa vyake vya kielekroniki.
Samsung
 Knox ni jukwaa la biashara la kupangilia na kudhibiti vifaa vya mkononi
 – ikileta ufanisi na kutoa matumizi mahususi katika sekta mbalimbali.
Huifanya miundombinu ya vifaa vya mkononi ikiwa imeunganishwa, salama na
 yenye tija. 
Tangu
 kuanzishwa kwake zaidi ya miaka kumi sasa, imefanikisha ulinzi wa vifaa
 vya Samsung takribani bilioni mbili na inatumika kusimamia vifaa zaidi
ya milioni 150. Ikiwa inaaminiwa duniani kote, Knox imesaidia biashara
zaidi ya 35,000 kufanikisha malengo yake kwenye mataifa tofauti.
Hivyo,
 ukiwa kama mtumiaji wa luninga za Samsung haupaswi tena kuwa na
wasiwasi kuhusu taarifa zako binafsi ulizoziingiza ili kunufaika na
huduma mbalimbali zinazotumia mtandao wa intaneti.
Samsung
 Knox hutambua kikamilifu matishio ya udukuzi yanavoweza kutokea kwa
wakati halisi, ikiripoti mabadiliko yoyote ambayo hayajaidhinishwa.
Inathibitisha kurasa tofauti za tovuti zinazofikiwa na watumiaji,
ikizuia kwa hiari tovuti hatarishi ili kulinda taarifa binafsi za
mtumiaji na faragha yake. Inahakikisha ulinzi thabiti wa taarifa binafsi
 za watumiaji kupitia muunganisho salama na Samsung Knox Vault,
kichakataji mahususi kwa usalama.
Luninga
 za Samsung zinalindwa dhidi ya hatari za uhalifu wa mtandaoni kutokana
na uwepo wa program ya Knox ambayo huifanya mifumo ya uendeshaji na
kifaa kuwa salama.
Unaweza
 kuwa unajiuliza kwanini ni muhimu kutumia luninga inayozingatia usalama
 wa taarifa zako binafsi. Lakini kumbuka kwamba ujio wa luninga za
kisasa umekuja na fursa ya matumizi ya huduma tofauti zilizounganishwa
na intaneti kama vile majukwaa ya mpira, filamu, michezo, burudani na
kuperuzi taarifa mbalimbali, ambazo kwa namna moja ama nyingine
zinahitaji uingize taarifa zako binafsi.
 
                         
                         
                         
                         
                         
                         
			
 
			 
			 
			