
PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 20,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 20,2024 Featured • Magazeti About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 20,2024 Featured • Magazeti About the author
Arusha. Tuhuma za kughushi nyaraka, uchepushaji wa makusanyo ya Serikali na ubadhirifu wa fedha za umma, zimekiweka shakani kibarua watendaji wa Jiji la Arusha wakiongozwa na Juma Hamsini. Mashaka hayo, yanatokana na amri ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwa Katibu Tawala wa mkoa huo, Missaile Mussa awasimamishe kazi watumishi hao kupisha uchunguzi…
Unguja. Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud amesema umefika wakati Wazanzibari kujiamulia na kupanga mipango yao wenyewe ili watu wake waishi kwa uhuru. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alitoa kauli hiyo leo Jumapili, Mei 19, 2024 wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho katika mikoa mitatu ya…
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kimbunga Ialy kinachovuma kaskazini mwa kisiwa cha Madagscar, ambacho awali kilidaiwa kingeishia baharini, kinaendelea kupata nguvu na kinatarajiwa kusababisha mvua kubwa na upepo mkali Tanzania siku ya Jumanne Mei 21, 2024. Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi leo Jumapili Mei 19,…
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, amesema Tanzania haitachoka kupeleka askari wake kulinda amani katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) kwa sababu inaamini katika uhusiano wa kindugu, uliowekwa na waasisi wa taasisi hiyo. Akizungumza na mabalozi wa nchi za Sadc wanaowakilisha nchi…
Na Mwandishi wetu, Arusha KAMPUNI ya Barrick nchini, imedhamini na kushiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC Tanzania) lililofanyika katika Chuo cha Uhasibu cha Arusha na kuwashirikisha wanafunzi, wahadhiri na wadau mbalimbali. Kupitia kongamano hilo ambalo hufanyika kila mwaka, wanafunzi huweza…
Dodoma. Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imeyatupa maombi ya askari wa Jeshi la Magereza aliyefutwa kazi mwaka 2022, Joel Runda Marivei ya kutaka Mahakama ifute uamuzi wa kumfuta kazi na mwajiri wake aamriwe kumrudisha kazini. Katika maombi hayo, Marivei aliyekuwa na cheo cha Sajini (Senior NCO) alimshtaki Kamishna Mkuu wa Magereza (CGP) kama mjibu maombi…
China imesema itaendelea kufadhili miradi mipya ya kimkakati ya Tanzania inayoendelea, baada ya kuridhishwa na utekelezwaji ya miradi ya awali. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Misaada la China (CIDCA), Luo Zhaohui, aliyasema hayo kwenye mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, yaliyofanyika jijini Beijing, China mwishoni…
Dar es Salaam. Wakati kukiwa na malalamiko ya kupanda kwa bei za bidhaa za chakula kutokana na kupaa kwa mafuta ya dizeli na petroli, huenda kilio hicho kikaongezeka baada ya ongezeko kubwa la gharama za usafirishaji wa mizigo kwa meli. Sababu ya ongezeko hilo inaelezwa ni ukosefu wa usalama katika safari za meli zinazotoka Ulaya…
Helikopta iliyokuwa imembeba Rais wa Iran, Ebrahim Raisi imeripotiwa kuanguka baada ya kupata shida katika kutua. Kwa mujibu wa televisheni ya Taifa ya Iran, helikopta hiyo imeanguka leo, Mei 19, 2024 karibu na Mji wa Jolfa, uliopo mpakani na Azerbaijan. Hata hivyo, taarifa hiyo haijaweka wazi chanzo cha moja kwa moja cha ajali hiyo, ingawa…