
ACT-Wazalendo yapanga kufumua mikataba, CCM yasema wanatafuta huruma kisiasa
Unguja. Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuna mikataba mingi mibovu inayoigharimu nchi na kwamba kikiingia madarakani mwakani kitahakikisha inafumuliwa na kuweka mipya. Kauli hiyo iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo-Zanzibar, Ismali Jussa imejibiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kikisema chama hicho hakina uwezo huo, bali kinalenga kupata huruma ya wananchi na kutafuta umaarufu wa kisiasa…