
Aliyekata rufaa kesi ya ubakaji mtoto, kufia gerezani
Kilimanjaro. Wahenga waliwahi kusema mtaka nyingi nasaba, hupata mingi misiba, ndiyo ujumbe unaoendana na kilichomkuta Emmanuel Steven baada ya Mahakama ya Rufani kuikataa rufaa yake na kubariki kifungo cha maisha jela alichohukumiwa kwa kumbaka mtoto wa miaka sita. Mbali na Jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo, Shaban Lila, Lugano Mwandambo na Lucia Kairo kubariki…