
CCM yawaonya tena wanaojipitisha ubunge, udiwani
Singida. Joto la uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 limeendelea kufukuta ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), huku Dk Emmanuel Nchimbi akiwaonya wanaopanga safu za wagombea au kujipitisha kuacha mchezo huo. Dk Nchimbi, ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM amesema hatua hiyo inawanyima usingizi viongozi waliopo kwenye dhamana kutekeleza wajibu wao….