
Wako wapi wanafunzi 538,526 waliotakiwa kufanya mtihani kidato cha sita?
Dar es Salaam. Wakati Serikali ikiendelea kutekeleza mpango wake wa elimu bila malipo, wadau wa elimu wanasema mzigo wa mahitaji binafsi ya mwanafunzi ni miongoni mwa changamoto inayowadondosha wanafunzi katika mfumo rasmi wa elimu. Takwimu za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) zinaonyesha wanafunzi 538,526 miongoni mwa 652,031 walioanza kidato cha…