
Hizi hapa athari za saa 36 za kimbunga Hidaya
Dodoma. Mvua zilizonyesha kwa takribani saa 36 zikiambatana na upepo mkali kutokana na kimbunga Hidaya zimesababisha vifo vya watu 10 na majeruhi saba, huku kaya 7,027 zenye watu 18,862 zikiathiriwa. Mbali ya hayo, nyumba 2,098 zimeathirika kati ya hizo, 678 zimebomoka kabisa, 877 zimeharibika kiasi, na 543 zimezingirwa na maji. Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu,…