
Bashungwa aapa kutoondoka Lindi, kisa barabara
Kilwa. Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema hatoondoka mkoani Lindi, hadi pale agizo lake la kujengwa kwa barabara iliyokatika kujengwa ndani ya saa 72 litakapokamilika. Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatatu Mei 6, 2024 alipotembelea eneo la Mto Matandu, Waziri Bashungwa amesema atajitahidi kufika maeneo yote yaliyopata madhara hata ikiwa kwa boti. “Kwa namna yoyote…