
SERIKALI YATOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 300 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU SHULE YA MSINGI TUNDURU MCHANGANYIKO
Na Mwandishi maalum,Tunduru. SERIKALI imetoa kiasi cha Sh.milioni 302 ili kuboresha mazingira na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi na walimu katika shule ya msingi Tunduru Mchanganyiko wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Sabina Lupukila amesema,kati ya fedha hizo Sh.milioni 246 zimetoka serikali kuu na Sh.milioni 56 zimetolewa na Halmashauri…