
Safari za baharini zarejea kimbunga Hidaya kikipoteza nguvu
Unguja. Baada ya kujiridhisha kuwa hali ya hewa imetulia na upepo kupungua, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeruhusu usafiri wa majini kuendelea kama kawaida. Usafiri wa meli na boti kutoka Unguja kwenda Dar es Salaam, Unguja kwenda Pemba na Pemba kwenda Tanga ulizuiwa tangu jana Mei 4, 2024 saa moja asubuhi kutokana na upepo…