
AKILI ZA KIJIWENI: Pamba mmerudi, ligi si kama mlivyoiacha
Wanetu wa Pamba FC aka Wana Kawekamo au ukipenda unaweza kuwaita TP Lindanda baada ya msoto wa muda mrefu hatimaye wamefanikiwa kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kushika nafasi ya pili kwenye Championship. Jamaa zetu wamesota sana kwani mara ya mwisho kwao kucheza Ligi Kuu ilikuwa ni mwaka 2001 ambapo tangu waliposhuka hapo hawajaweza…