
Watuhumiwa wengine sita wabainika ubadhirifu wa Sh1.3 bilioni
Mbeya. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Mbeya imebaini ongezeko la watuhumiwa sita wa ubadhirifu wa fedha kwa njia ya mtandao (POS) huku kiwango cha fedha kikipanda kutoka Sh382 milioni hadi Sh1.3 bilioni. Agosti 28, 2023 zaidi ya watu 40 wakiwamo madiwani, watumishi, watalaamu wa Tehama na watendaji wa kata walishikiliwa…