
Wafanyabiashara Kariakoo walia kuzingirwa na majitaka
Dar es Salaam. Wananchi wa Mtaa wa Lindi Kata ya Gerezani Kariakoo wamesema wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kwa kuwa maeneo wanayofanyia biashara zao kuzungukwa na maji machafu yaliyo changanyika na vinyesi. Wananchi hao wanaofanya shughuli zao hizo karibu na stendi zinapoegeshwa daladala za Gerezani -Buza wamesema wanashangaa kuona wanatozwa ushuru lakini usafi hauzingatiwi…