
Mkutano wa mwaka wa WHO waanza Geneva – DW – 27.05.2024
Wanachama 194 wa WHO wanapanga kuanzisha miongozo ya vipaumbele vya miaka minne ijayo, ikiwa ni pamoja na mpango wa kuiondoa kabisa Malaria katika baadhi ya mataifa ifikapo 2030, lakini pia hatua ya kukabiliana na ongezeko linaloibua kitisho la usugu wa bakteria, fangasi, virusi, na vimelea. Hafla ya kutiliana saini mkataba wa WHO kuhusu majanga, iliahirishwa…