
Serikali imeonyesha nia nje, kazi kwa TFF
WIKI iliyopita Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo iliwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi yake kwa mwaka 2024/25 yaliyoonyesha ongezeko kubwa la zaidi ya asilimia 700 kutoka bajeti yake iliyozoeleka iliyokuwa ya takriban Sh35 Bilioni. Bajeti ya safari hii imefikia Sh285.3 Bilioni ukilinganisha na ya mwaka uliopita wa fedha iliyokuwa Sh35.4 Bilioni. Akiwasilisha bajeti…